Opening the chapter…
Gloryian · © Guini Productions LLC
Zaburi ya Daudi. Zaburi. Amebarikiwa mtu yule aliyesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimesitiriwa.
Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe hamuhesabii hatia na ambaye rohoni mwake hamna udanganyifu.
Nilipokaa kimya, mifupa yangu ilidhohofika huku nikiugua muda wote.
Mchana na usiku mkono wako ulinielemea. nguvu zangu zilikauka wakati wa kiangazi. Selah
Ndipo nilipotambua makosa yangu kwako, nami sifichi tena uovu wangu. Nilisema, “Nitakiri makosa yangu kwa Yahwe,” nawe ulinisamehe hatia ya dhambi zangu. Selah
Kwa sababu ya haya, wale wote ambao ni wa kimungu wanapaswa kukuomba wakati wa shida kubwa. Nayo mafuriko yajapo, hayatawapata watu hao.
Wewe u mahali pangu pa kujifichia, nawe utanilinda matatizoni. Wewe utanizunguka pamoja na nyimbo zaushindi. Selah
Nitakuelekeza na kukufundisha katika njia upasayo kuiendea. Nitakuelekeza huku macho yangu yakikutazama.
Msiwe kama farasi au kama nyumbu, ambao hawana uelewa; ni kwa hatamu na lijamu tu unaweza kuwapeleka popote utakapo wao waende.
Waovu wanahuzuni nyingi, bali uaminifu wa agano la Yahwe utamzunguka yule anaye mwamini yeye.
Furahini katika Yahwe, na mshangilie, ninyi wenye haki; pigeni kelele za shangwe, ninyi nyote wenye haki mioyoni mwenu.
Biblia Takatifu, Swahili Unlocked Literal Bible. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Licensed under CC BY-SA 4.0 (https://creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0/). Source: eBible.org (swhulb). Changes: reformatted for display (USFM to verses); no wording changed. Audio and other adaptations are shared under CC BY-SA 4.0.
Sign in to hear David
Sign in