Opening the chapter…
Gloryian · © Guini Productions LLC
Mungu amefanya mwenyewe kujulikana katika Yuda; jina lake ni kuu katika Israeli.
Hema yake iko salemu; makao yake yako yako Sayuni.
Huko ndiko alivunja mishale ya upinde, ngao, upanga, na silaha zingine za vita. Selah
Wewe unang'aa sana na huufunua utukufu wako, ushukapo kutoka milimani, ambako uliwauwa mateka.
Wenye moyo shujaa walitekwa nyara; walilala mauti. Mashujaa wote walikuwa wanyonge.
Kwa kukemea kwako, ewe Mungu wa Yakobo, wote gari na farasi walilala mauti.
Wewe, ndiyo wewe, ni wa kuogopwa; ni nani awezaye kusimama mbele yako wakati ukiwa na hasira?
Kutoka mbinguni wewe uliifanya hukumu yako isikike; nchi iliogopa na ikaa kimya
wakati wewe, Mungu, ulipoinuka kutekeleza hukumu na kuwaokoa wote wa nchi walio onewa. Selah
Hakika hukumu ya hasira yako dhidi ya binadamu itakuletea wewe sifa; wewe hujifunga mwenyewe hasira yako iliyo baki.
Wekeni nadhiri kwa Yahwe Mungu wenu na kuzihifadhi. Nao wote wamzungukao yeye mleteeni zawadi yeye ambaye ni wa kuogopwa.
Yeye huzikata roho za wakuu; huogopwa na wafalme wa nchi.
Biblia Takatifu, Swahili Unlocked Literal Bible. Copyright © 2019 Door43 World Missions Community. Licensed under CC BY-SA 4.0 (https://creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0/). Source: eBible.org (swhulb). Changes: reformatted for display (USFM to verses); no wording changed. Audio and other adaptations are shared under CC BY-SA 4.0.
Sign in to hear David
Sign in